Wednesday, August 16, 2017

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 11

 
Image result for sorry madam

ILIPOISHIA
 

.....Manka akamaliza kuvuta sigara yake kisha akatoka chumbani huku bastola yake ikiwa mkononi.Nikaona nikiendelea kujilaza kitandani utakuwa ni ujinga wa karne.Nikajivuta juu kidogo na kuanza kuifungua kamba ya mkono wa kulia kwa kutumia meno japo ninapata maumivu ila nikayapotezea,Nikafanikwa kuifungua kamba kisha kwa haraka nikaifungua kamba ya kumkono wa pili na kumalizia kamba za miguuni kala sijanyanyuka kitandani nikajikuta tunatazamana na Manka huku bastola yake akiwa amenielekezea kwangu.Nikamrukia Manka kabla hata sijamfikia nikstukia kitu chenye ncha kali na chamoto kikipenya ndani ya kifua changu na kuningusha chini.....

ENDELEA....
.....Maumivu makali yakanitawala katika kifua changu nikajishika kwenye kifua changu na kugungua kuna damu zinanitoka ikanibidi niukaze mkono wangu ili kuzuia damu nyingi kuendelea kuvuja katika sehemu risasi ilipo pita.Manka akaanza kuweseka huku akiwa kama haamini kwa tukio alilo lifanya.Akaitupa bastola chini na kupiga magoti kuangalia eneo aneo alilo nijeruhi kwa risasi

“Eddy nilikuwa ninakutania”
Manka alizungumza huku akilia na kuonekana kuchanganyikiwa kwa kitendo alicho nifanyia.Taratibu nikahisi nguvu zikiniishia huku mwili ukizizima kwa kukosa uwezo wa kufumbua machona taratibu nikajikuta hali nzito ambayo sikuwahi kuipata katika maisha yangu ikiutawala moyo wangu.

                                           ***
 Macho yangu yakafunguka na kujikuta Mama akiwa amekaa pembeni yangu huku puani kwangu nikiwa na mashine ya kupulia.Mama alipo niona nimefungua macho yangu akaanza kuliita jina langu na nikamuitikia kwa sauti ya chini

“Mwanangu unajisikiaje?’
Nikataka kunyanyuka ila nikashindwa na mama akanirudisha chini na kugundua kuna bandeji kuwa nimefungwa kwenye kifua changu.Kumbukumbu zinanikumbusha dakika za mwisho nilikuwa na Manka ila kuanzia hapo sikuelewa kitu kilicho enedelea hadi mama akawa pembeni yangu.

“Mama nipo wapi?”
“Mwanangu upo hospitalini?”
“Nani kanileta?
“Ni story ndefu kidogo mwanangu ila kwa sasa pumzinka nitakuadisia ukipata nafuu”

   Simu ya mama ikaita akaitazama kwa muda kisha akaipokea na nikamuona sura yake ikiwa imebadilika kidogo na kuwa sura ya hasira

“Ndio ameamka”
“Godwin nakuomba unielewe hapa huna mtoto na huyo mwanao aliye mfanyia mwanangu hivi nilazma nimfunge”
“Ahhhh kwahiyo wewe ndio umemtuma amuue mwanangu si ndio?”

“Sasa lazima nimfunge na kumbuka kuwa tangu mwanangu akiwa utotoni hukuwa na mapenzi naye sasa naomba umuache na wala sihitaji urudi uje umuuone”

 Mama akakata simu huku akiachia msunyo mkali,sasa sikuelewa anazungumza na nani na kumfokea kiasi hicho
“Mama unazungumza na nani?”
“Ahaaa mwanangu nitakuambia”

Mama alanijibu huku akiwa anatabasamu kisha akanibusu katika paji la uso wangu.Simu yake ikaiita tena na ikamlazimu kutoka nje.Sikutaka kujisumbua mama anamfokea nani niahisi watakuwa ni watu wa serikali anao fanya nao kazi.Mama akarudi na kukaa karibu yangu huku machozi yakimlenga lenga akionekana kuwa na hasira kubwa na tangu nizaliwe sikuwahi kumuona mama akiwa katika hali kama hiyo.

“Mama nipo hospitali gani?”
“Ni KCMC”
 Mlango ukafunguliwa akaingia mzee wa makamo akiwa amevalia nguo za polisi huku akiwa na vyeo vingi
“Habari yako mheshimiwa?”
“Salama vipi mumesha mkamata aliye sababisha hili tukio?”

“Ndio muheshimiwa ila ninashindwa kuelewa kwani mzee ananiambia nimuachie huru ili we……”
“Nisikilize wewe mimi si ndio nimetoa  amri yule binti kukamatwa?”
“Ndio”
“Sasa mbona unaniletea Kiswahili.Muwekeni ndani hadi mimi nije sawa”
“Sawa mkuu”

Askari akatoka na kutuacha ndani ya chumba na ukimya ukatawala huku mama akonekana kusongwa na mawazo na mara kwa mara akawa anasunya sikujua kinacho mfanya asunye ni nini.

 Nikakaa hospitali kwa wiki moja nikapewa ruhusa japo sikuwa nimepona vizuri.Safari ya kwenda uwanja wa ndege wa KIA ikaanza huku dereva anayemuendesha mama akiwa makini katika uendeshaji wake kutokana Dokta ameniambia nisifanye kazi ngumu wala kupata mitingishiko ya aina yoyote kwani kidonda changu kinaweza kisipone kwa haraka.Tukakuta ndege ya kukodi ikiwa tayari kwa ajili yetu mimi na mama.Tukapanda na dereva akaondoka na gari ya mama na tukaahidiana naye atatukuta nyumbani.Safari ikaanza taratibu huku ndege aina ya Fast Jet tuliyoipanda ikizidisha kasi kadri muda unavyo kwenda tukiwa angani

  “Pole kaka”,Muhudumu wa kike wa ndege akanipa pole huku akiniwekea juisi kwenye kimeza kidogo kilichopo mbele yangu
“Asante”
“Muheshimiwa huyu ni mwanao”
“Ndio ni mwangu wa kwanza na wamwisho”
“Aisee mtu akikutizama wala hata amini kama unamtoto mkubwa kiasi hichi”

“Unajua kipindi sisi tulipokuwa tunamaliza kidato cha sita mika ya themanini tulipelekwa jeshini sote na ilitusaidia kuweza kuzilinda afya zetu ni tofauti na hao kina Eddy mtu nikimwambia mwanangu ana miaka 20 haamini”
“Mmmm mama umekosea nina miaka 21”

“Sasa sibado haijatimia”
“Sasa muheshimiwa nyinyi si mupo huku ngazi za juu kwanini musirudishe sheria ya wanafunzi wanao maliza kuingia jeshini?”

“Ile imerudishwa sasa sijui huku mwanagu kama ataweza kwa maana mmmm”
“Mama wewe unaniona mimi nimeoza sana”
“Wewe hujioni”

Tukacheka sote na safari ikaendelea,haikuchukua muda sana kutua katika uwanja wa ndege wa mwalimu JK Nyerere.Gari ya serikali ikaja kutuchukua na kutupeleka nyumbani maeneo ya Masaki.Nikakumbuka kuna kitu ninakihitaji kukijua vizuri kutoka kwa mama kwani kila nilipohitaji kumuuliza nilijikuta nikisahau

“Mama hivi pale hospitalini nilifikaje?”
“Eddy mwanagu hata hatujapumzika umeanza kwa maswali?”
“Ndio ama nataka kujua?”
“Kavue nguo zako chumbani kwako upumzike kisha wakati wa jioni tutazungumza ngoja mimi niende ofisini jana kuna kazi niliiacha”

“Kwani mama jana ulikuja ofisini?”
“Ndio kila siku nilipokuwa ninakuja hospitali nilikuwa ninalala Dar asubuhi ninakuja kwa ndege jioni au mchana ninarudi kwa ndege”

“Mmmmm mama mbona nyumba ipo kimya dada wa kazi yupo wapi?”
“Nimemfukuza”
“Kwa nini?”
“Nitakuja kukuambia jioni nikitoka kazini”

Mama akaondoka mimi nikaelekea chumbani kwangu,sikukuta kuna mabadiliko ya aina yoyote tangu nilipo kiacha pindi nanakwenda shule.Nikaingia bafuni nichukua taulo na kulichovya kwenye maji na kuanza kujisujgua sehemu ya mwili kwani ndio oga yangu tangu nikiwa huspitalini hii ilisaidia kidonda kuto kuingia maji.Nikamaliza na kurudi kitandani kutokana nimeshiba nikaamua kulala.

Nikaamka mida ya saa moja jioni na kutoka chumbai kwangu na kumkuta mama akiwa anaandaa chakula.Nikamsalimia na kukaa kwenye moja sofa zilizopo katika sebule yetu.

“Umekunywa zile dawa za kutuliza maumivu?”
“Hapana?’
“Kwa nini wakati unatakiwa kuzinywa kila jioni?’
“Mama sibado sijala.Nikila nitameza”
“Unanjaa nikupakulie chakula?”

“Mmmm nitakula baada ya kuzungumza na wewe”
“Eddy yaani mwanangu ukishikilia bango kitu yaani hadi kikamilike”
“Ila mama hiyo tabia si nimeridhi kwako”

“Kwenda zako mimi sina tabia za king’ang’anizi kama wewe”
    Mama alizungumza huku kija kukaa karibu yangu na kuanza kukichunguza kidonda changu kikiwa ndani ya bandeji kubwa iliyo zungushwa nusu kufua na kufungiwa kwa mgongoni

“Alafu hicho kidonda ukikitia maji kitachelewa kukauka”
“Sijakitia….eeehe mama kwanza swali langu la mimi nimefikaje pale hospitalini ujanijibu hadi leo?”

“Pale hospitalini ulipelekwa na wasamaria wema ambao walikuokota pembezoni mwa mto huku ukiwa umevalia suruali ya jeans na ulikuwa kifua wazi.Kwa mashuhuda nilio zungumza nao katika kituo cha polisi waliseama ulitupwa mida ya saa kumi na moja asubuhi na binti aliyekuwa na pikipiki”

“Sasa ikawaje?”
“Kuna bibi alikuwa yupo na mjukuu wake wa kiume walikuwa wakielekea shamba ndio wakakuona pembezoni ya mto huku mtu waliyemuona akiwa anakimbia na pikipiki……Unamjua mtu huyo?”

 Swali la mama likaniweka njia panda huku nikijiuliza maswali ni nini nimjibu mama kwani nikisema nina mjua ataniuliza ni nani na nikisema simjui atasema nilikuwa ni wapi ninatoka wakati wa usiku

“Ninamjua”
“Ahaaa basi baada ya watu hao kukuwahisha hospitalini kwani hali yako ilikuwa mbaya sana ikawalazimu madaktari wapewe namba ya baba yako na mmoja wa waalimu aliyedai ni shemeji wa yule binti kisha baba yako ndio akanipigia mimi”

“Alafu mama nilikusikia kama ukibishana na simu kuwa kuna mtu alimtuma yule binti aniue?”.Mama akakaa kimya huku akinitazama kwa macho yaliyojaa masikitiko na kwa mbali machozi yakaanza kumlenga lenga.

“Mwanangu kuna historia ndefu sana unatakiwa kuijua ila kwa kipindi hiki nakuomba usome kwa juuhudi sana na uaache michezo”

“Mama na hisoria gani?”
“Utakuja kuijua tuu”
“Mama nataka kuijua kwani mama una mtoto mwengine zaidi yangu wa kumwambia mambo yanayohusu familia yetu?”

 Mama akanitazama kwa macho yaliyo jaa uchungu na machozi yakaanza kutapakaa kwenye uso wake na kunifanya na mimi nimpokee kwa machozi yalioanza kunichuruzika na kwa mistari mistari kwani mara ya mwisho kumuona mama analia ni miaka kumi iliyopita siku ya kifo cha mama yake.

“Eddy nakuomba uwe na moyo na koo la kuvumilia hiki nitakacho kuambia kwani kinahitaji moyo wa ujasiri na nisiri ambayo sijawahi kumuambia mtu wa aina yoyote zaidi yako na ninakuambia hivi kwa sababu wewe ni mwangu wa pekee”
“Niaimbie mama”

“Eddy nilikutana na baba yako kwenye ajali moja ya basi iliyotokea kipindi mimi ninaelekea chuo katika kumaliza mafunzo ya mwisho ya udaktari.Katika ajali ile watu wengi walijeruhiwa na kama sijakosea ni watu wawili tuu walipoteza maisha.Mimi namshukuru Mungu sikupata majeraha makubwa zaidi ya michubuko midogo midogo ila kwa upande wa baba yako yeye alipata majeraha makubwa sana katika maeneo ya kiunoni na kutokana mimi nilikuwa ni daktari wa upasuaji basi nilijumuika na madaktari wezangu kumfanyia baba yako upasuaji chini ya kitovu ambapo tulikuta mirija yake ya uzazi imeharibika na tukashauriana na madaktari wezangu ambao walinishangaa kuniona nina uwezo mkubwa wa kumfanyia mtu upasuaji japo kuwa nilikuwa bado ni mwanafunzi tukaona ni vyema tukamtoa……..”

Mapigo ya moyo yakanipasuka na kujikuta nikikaa vizuri kwenye sofa na kumtazama mama ambaye uvumilivu unamshinda na kujikuta akiendelea kutokwa na machozi.Mama akameza fumba la mate kisha akaendelea

“Tuliichoma sindano mirija yake ya uzazi ili kuwatoa bacteria ambao wangeweza kushambulia mirija hiyo kwa jinsi ilivyokuwa imeharibika.Lakini mwanangu kusema kweli ile sindano haikuwa nzuri kutokana inamfanya mwanaume kukosa uwezo wa kuzalisha mbegu zenye nguvu zitakazo mpelekea mwanaume kumzalisha mwanamke”

 Nikajihisi mwili mzimwa kupoteza nguvu kutokana na maelezo ya mama na moja kwa moja hisia za baba niliye naye sasa hivi si baba yangu zikaanza kuutawala moyo wangu na kujikuta nikiwa mapigo ya moyo yakianza kunienda kwa kasi hadi na kwa maumivu ya kifua yanayotokana na jeraha la risasi yakanisababishai kizungu zungu kikali kilichonipelekea kujilaza kwenye kochi na nikaanza kuliona giza kubwa likitawala macho yangu kama ilivyokuwa siku niliyo pigwa rasasi na Manka....

Related Posts

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 11
4/ 5
Oleh