
ENDELEA...
....Nikabaki nimesimama huku sielewi ni kitu gani nifanye nikageuka kiunyonge na kukutana na daktari tuliyemkuta jana usiku akiwa anatembea mwendo wa kasi sikujua ni wapi anapoelekea ikanibidi nimsimamishe.
....Nikabaki nimesimama huku sielewi ni kitu gani nifanye nikageuka kiunyonge na kukutana na daktari tuliyemkuta jana usiku akiwa anatembea mwendo wa kasi sikujua ni wapi anapoelekea ikanibidi nimsimamishe.
“Daktari vipi”
“Salama mdogo wangu nakomba tuzungumze baadaye mimi ngoja niondoke hali imeshakuwa mbaya”
“Sijakuelewa dokta?”
“Kuna waziri wa afya amekuja hapa tayari dokta mkuu ameshapigwa chini wewe nakuomba tuondoke kama vipi njoo tuzungumze nyuma huku”
Nikatoka huku nikicheka kimoyo moyo na kusema laiti angejua huyo mtu anaye mkimbia ni mama yangu wala asingezungumza na mimi.
“Ehee kijana shida yako ni nini?”
“Dokta jana nilileta mgojwa hapa mida wa usiku alipatwa na….”
“Ohooo nimekumbuka huyo mgonjwa wako tumemsafirisha kuelekea katika hospitali ya K.C.M.C”
“Hali yake ikoje?”
“Si nzuri sanaa na kama tungembakisha hapa angetufia bure…..Kijana hebu nakuomba uniache niende kwani huyo mama namuona anakuja huku”
Dokta alizungumza huku akichungulia chungulia kupitia mlango tulio tokea nje huku akianza kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye njia ya kichochoro iliyopo karibu na Zahanati hiyo.Nikarudi ndani huku nikiwa nawaza ni nini nifanye ili mama aweze kunielewa kama ni kuenda shule niende siku hiyo hiyo.Mama akamaliza kuzungumza na madaktari pamoja na manesi aliowakuta.
“Ehee wee huyo mgonjwa wako yupo wapi?”
“Wamesema wamemuamisha hospitali”
“Nani kasema?”
“Waulize hao madokta hapo”
“Eti kuna mgonjwa aliletwa jana amepata ajali?”
“Ndio muheshimiwa”
“Ahaa bahati yako haya jamani tekelezeni yale niliyo waambia ni bora mupoteze kazi nyingi kuliko kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa vifo vinavyosababishwa na uzembe wenu na kuanzia sasa hivi Kiongozi mkuu atakuwa huyo hapo bwana nani vile?”
“Bwana John Henry”
“Ok bwana John ndio atakuwa kiongozi wenu kwa muda hadi pale wizara itakapo leta mtu daktari mwengine sawa jamani.”Madaktari na Manesi wakamuitikia mama kisha akaagana nao pamoja na wananchi kisha tukaingia ndani ya gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.Tukafika nyumbani mida ya saa saa nane mchana.Wakanishusha getini kisha mama akaelekea kwenye mishuhuliko yake.Mida ya jioni mama akarudi huku akionekana amechoka nikamsalimia na moja kwa moja akaenda chumbani kwake na kulala.Nikakaa nyumbani kwa siku mbili na bila ya kuzungumza na mama kuhusiana na swala la kurudi shule.
“Eddy shule unakwenda lini?”
Mama aliniuliza baada ya kupita mbele yake nikitokea nje huku yeye akiwa amekaa sebuleni akitazama taarifa ya habari ya saa mbili usiku
“Mama nakusikilizia wewe?”
“Unanisikilizia mimi hivi unaakili kweli mwanangu?”
“Sasa mama kuzungumza hivyo ndio mimi sina akili?”
“Nakuona bado unaakili za kitoto.Sasa anaye soma ni mimi au wewe?”
“Ila kumbuka mama wewe ndio uliye niruduisha nyumbani”
“Nilikurudisha ili akili yako ikae sawa.Na sijui hiyo PCB yako unaisoma vipi?”
“Mama mimi Genius”
“Mmmm genius uwe wewe,kesho shule na uondoke na gari ya kwanza uwahi kufaika shuleni?”
“Mama siwezi kusafiri ijumaa”
“Pumbavu wewe usiniletee ujinga nimekuambia kesho alfajiri nikitoka kwenda kazini ninakuacha ubungo sawa”
“Ila mama hizi safari zako za kushtukiza huwa sizipendi kama nini”
“Upende usipende kesho shule”
Kama alivyozungumza mama safari ya kurudi shule ikaanza na akaniacha stendi ya mabasi ya Ubungo mida ya saa kumi na moja asubuhi kisha yeye akaelekea ofisini kwake sikujua ni kwanini siku hiyo amewahi sana kwenda ofisini.Nlicho kifanya ni kutafuta nyumba ya wageni(gest house) iliyo karibu na stendi kwa bahati nzuri nikapata chumba nikaingia na kulala hadi mida ya saa tatu asubuhi kisha nikarudi stendi na safari ikaanza kwa kutumia basi Dar Express na katika siti niliyokaa nipembeni yangu kuna msichana amavalia baibui ninja na ni ngumu kuweza kuiona sura yake.
Hatukusemeshana chochote kiasi kwamba safari nzima kila mtu akawa kimya,kwa bahati mbaya tukakuta ajali ya roli mbili zimegongana maeneo ya Wami kiasi kwamba ikatuchukua muda mrefu kukaa barabarani tukisubiria gari hizo kuja kuondolewa kutokana zimeifunga barabara na hapakuwa na uwezekano wa magari kupita.
“Aisee hii ajali inatuchelewesha”
Msichana niliye kaa naye alizungumza na kunifanya nimtazame kwa muda kisha nikamjibu.
“Wee acha tuu yaani nilisaa la tatu tumekaa hapa na hiyo foleni hapa hadi tuimalieze ni shughuli”
“Ndio tatizo la nchi yetu kukitokea jambo kama hili basi wahusika wataanza kujivuta vuta usishangae hapa tunakaa zaidi ya masaa kumi”
“Kweli na hapa mtu huwezi kusema utahairisha safari kwani nyuma yetu kuna foleni mbele huko ndio usiseme”
“Kuna biashara zangu nilitaka kuziwahi ila hapa nimesha chelewa itanilazimu kulala Arusha kitu nilichokuwa sijakipanga kabisa”
“Ulitaka urudi leoleo?”
“Ndio ila kwa hali hii nahisi hapa kuna kulala”
“Wewe ni mfanya biashata?”
“Ndio ninachukua mizigo ya nguo za wanawae na watoto kutoka Dar na kwenda kuuza Arusha”
“Ahaa hivi hiyo biashara inalipa?”
“Ina lipa pale mtu unapokuwa mchacharikaji ila ukiwa goigoi utaiacha kazi…..Vipi wewe uanashughulika na nini?”
“Mimi ni mwanafunzi nipo kidato cha tano”
“Ahaaa ila si hamjafunga bado?”
“Ndio ila mimi kuna matatizo kidogo yalinipata ndio nikarudi nyumbani ila sasa hivi kidgo nipo powa”
“Soma bwana sisi wengine tulikimbia shule na sasa hivi tunazunguka zunuka na dunia”
“Sawa ila hata wanao soma pia wanaangaika na dunia”
“Ni kweli ila huwa ninawashangaa sana wale wanaosoma na kutaka kuajiriwa.Wanashinda kutumia elimu walizonazo katika kubuni miradi itakayo waingizia pesa wanakazi ya kukaliaa kuhangaika na vijibahasha vyao kwenye maofisi ya watu na mbaya zaidi unakuta mshaara anaolipwa ni waajabu sana”
“Yaani wee acha tuu mdoi maana mimi katika maisha yangu sijapanga kuja kuajiriwa nahitai nijiajiri mimi mwenyewe”
“Ukiwa na nia na malengo utaweza hakuna kinacho shindikana chini ya jua”
Gafla tukasikia mlipuko mkubwa ukitokea katika magari ya mbele ya magari yetu na ikatulazimu tushuke kwenye gari haraka kwenda kuangalia ni nini.Tukakuta moshi mwingi mweusi ukisambaa angani na huku magari mawili ya mbele ikiwemo roli la mafuta lililopata ajali yakiteketea kwa moto mwingi.Watu waliopo kwenye magari ya karibu na magari hayo yanayowaka moto wakaanza kukimbia kurudi nyuma tulipo sisi na kusababisha msongamano mubwa wa watu wanao jaribu kuziokoa roho zao.
“Huu moto utakuja tuu huku”
Msichana alizungumza huku akiwa anafunua kitambaa kilicho iziba sura yake na kujikuta nikimeza fumba kubwa la mate na kubaki nikimtazama jinsi alivyojaliwa uzuri wa sura kiasi kwamba nikajikuta nashindwa kumjibu kitu
“Vipi mbona unanishangaa?”
“Ha…haaa pana”
Kabla sijajibu chochoye gari nyingine mbili zikashika moto na kuanza kuteketea na kwa mahesabu ya haraka haraka gari letu ni la nane kutoka katika gari nne zinazoteketea kwa moto.Polisi wa kikosi cha barabarani wakaanza kuwaomba watu kurudi nyuma kwani hali sio nzuri na muda wowote magari mengine yanaweza kufwata katika kuungua kwa moto.Nikaingia ndani ya basi na kuchukua begi langu la nguo pamoja na pochi kubwa ya msichana huyo kisha nikashuka na tukajumuika na watu wengine kurudi nyuma huku tukizipisha gari za zima moto kufanya kazi yao.
“Kaka unaitwa nani?”
“Ninaitwa Eddy wewe je?”
“Mimi ninaitwa Sheila”
“Una jina zuri”
“Hahaaaaa wapi mbona jina la kawaida”
“Ebwaane ehee hapa safari inaweza ikaahiriswa?”
“Sijui tusubirie matoke kwa maana hapa hali imeshakuwa mbaya”
Kazi ya kuuzima moto unaowaka ikaanza kuwashinda wazimaji kwani magari mengine yakaanza kushika moto kwa kasi na mbaya zaidi katika eneo tulilokuwepo upepo wake ni mkali kiasi kwamba husababisha moto huo kuyapata magari mengine.Watu baadhi wakaanza kupanda boda boda za pikipiki kuondoka katika eneo hilo huku watu wengine wakiyalilia magari yao yanayo teketea kwa moto na kujikuta nikaanza kumcheka jamaa mmoja anayelia.
“Eddy unacheka nini?”
“Yule jamaa pale aliye kaa chini kwenye majani ameunguliwa na ile Nohah yake kule mbele”
“Ndio unamcheka mwenzoko?”
“Hapana ninachokicheka mimi ni maneno yake anadai gari ameichukua juzi kwa mkopo wa benki alafu leo limeungua moto”
“Masikini wee kaka wa watu hadi huruma”
“Kweli anatia huruma ila vitu vya mkopo vinapo pata majanga kama haya hukufanya upagawe na kulia kama mtoto mdogo”
Tukaendelea kukaa kwa masaa matatu mbeleni ila matumaini yetu yakaanza kupotea taratibu huku sote tukishuhudia basi letu likiwa ni miongoni mwa magari yanayo teketea kwa moto.Nikiwa nimeduwaa simu yangu ikaita na kukuta mama ndio anaye piga.
“Wewe umeshafika wapi?”
“Mama ndio tunakaribia kuingia Moshi”
Ikanilazimu kukaa kumdanganya mama kwani tangu ninaondoka nyumbani alikuwa akinisema sema na kuniona mimi ni mzembe wa kutokupenda shule isitoshe aliniambia niondoke na gari la kwanza kwenda Arusha mida ya saa kumi na moja alfajiri ila kwa uzembe wangu nikaondoka na gari la saa nne asubuhi.
“Ahaaa nilijua umekwama hapo WAME”
“Hapana tumepapita muda mrefu sana hapo wami kwani kuna nini?”
“Kuna magari yamepata ajali hapa natazama breaking news kwenye Tv ndio maana nikakuuliza”
Moyo ukanipasuka kwani katika sehemu niliyo kuwepo kuna Camera za waandishi wa habari ila sikujua ni waandishi wa kituo gani cha habari.
“Haya mama simu yako inakata kata sikusikii vizuri “
Mama akakata simu ikanibidi nimshike mkono Sheila na kusimama naye mbali kidogo na walipo waandishi wa habari
“Vipi mbona ngija ngija za kuvutana?”
“Ahaa nimeamua tuje tusimame huku nifanye mpango wa kutafuta pa kwenda kulala ka maana hapa naona safari hakuna tena”
“Si urudi nyumbani?”
“Nyumbani hakurudiki itanilazimu nikalale hoteli”
“Mmmm basi fanya hivyo ngoja mimi nione kama kuna uwezekano wa kuendelea na safari”
“Sidhani kama utaweza kuendelea na safari”
“Eddy mbona unanikatisha tamaa?”
“Sikukatishi tamaa ila ndio ukweli wenyewe”
“Powa basi twende kwangu”
“Kwako?”
“Ndio unaogopa nini kwani?”
“Siogopi ila nisije nikavunjwa meno tu”
“Uvunje meno na nani?”
“Na wanao miliki mali yao”
“Hakuna kitu kama hicho”
“Sawa”
Tukapanda boda boda za pikipiki hadi chalinze na tukakodi taksi hadi nyumbani kwa Sheila maeneo ya Kimara na tukasimama mbele ya nyumba ya kifahari nyenye geti kubwa.Sheila akamlipa dereva taksi kisha tukashuka akafungua geti na kuingia ndani na nyumba imetawaliwa na ukimya mkubwa
“Mbona kupo kimya?”
“Ninaishi peke yangu”
“Kumbe unamaisha mazuri hivi?’
“Wapi nimepanga tuu hapa”
Tukaingia ndani na Sheila akanikaribisha kwenye sofa zake na kunipa kunipa maji ya baridi kisha yeye akaingia ndani.Kutokana kupo kimya sana nikaona ni bora niwashe Tv iliyopo hapo sebleni na nikachagua CD zilizopo juu ya spika za redio na kuipata CD moja isiyo na maandishi ya aina yoyote wala kuwa na picha.Nikaiweka kwenye deki kisha nikapunguza sauti hadi mwisho kwani ninakumbuka yaliyo nikuta kwa Madam Mery kwa kukuta CD ya ngono.
Kajasho kembamba kakaanza kunimwagika baada ya kuona CD hiyo ikionyesha mazingira ya humu sebleni na katika kochi nililo kaa mimi kulikuwa na jamaa amekaa huku akipiga kelele na akionekana analia kama mtoto mdogo.Camera ikashushwa chini kidogo na nikaona jamaa akivuja damu nyingi sehemu zake za siri kiasi kwamba damu zikaanza kunisisimka.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio baada ya kumuona msichana akiwa amesimama mbele ya kamera huku akiwa uchi na mkononi mwake akiwa ameshika uume wa mwanaume uliokatwa.
Mwanamke huyo akaishika kamera na kuipandisha juu kidogo na kuiona sura Sheila huku akiwa ametabasamu na kuzungumza maneno yaliyozidi kuniogopesha
“KILA MWANAUME KWANGU NIKITEGA UCHUMI HAHAAAAAAAAAAAAAA…………”
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 17
4/
5
Oleh
Unknown