
Muda: usiku Ikiwa ni kipindi cha mvua zinaendelea kunyesha. Katika moja ya mitaa tulivu kuna nyumba moja kunaonekana ndani kuna ugomvi kati ya mwanamke na mwanaume lakini mwanamke anaonekana akiwa kaelemewa. Matukio yote haya yanaonekana kupitia dirisha la vioo ambalo panzia yake imekaa upande na kufanya ndani kuonekane. Bado ugomvi unaendelea kati yao, mara mwanamke anachoropoka mikononi mwa mwanaume na kukimbia, anafungua mlango na kutoka nje mvuani anakimbia huku akilia . Mwanaume alitoka na kumkimbilia huku akimwita lakini alimkosa akarudi ndani huku akigeuka kumtazama.
(closing scene) Scene 1 Mahali: (jikoni) nyumbani Wahusika: nadya na mzimu wa shadya
Muda: mchana Sehemu ya sebule ya nyumba hii inaonekana kuwa kimya kiasi, kunaonekana kama kuna mtu akiangaza kila mahali haonekani ni nani , akawa anaelekea jikoni ambapo nadya anaonekana akipika. Taratibu yule mtu akaanza kumnyatia nadya kisha akampuliza nywele kwa nguvu, alipogeuka nadya hakumuona mtu akaanza kushangaa, ndipo akasikia tv ikifoka ghafla, taratibu akatoka jikoni na kuelekea sebuleni kutazama ni nani lakini hakumuona mtu yeyote, akazima tv na kurudi jikoni lakini baada ya kuzima kuna mtu anaonekana kivuli chake kwenye kioo cha tv lakini nadya hakumuona kuna nani, akaenda kuendelea na kazi zake.
Scene 2 Mahali: bafuni, chumbani Wahusika: nadya, mzimu wa shadya na morey Muda: jioni Nadya akiwa anaoga bafuni ghafla wakati anapeleka mkono mgongoni kuna mkono wa ajabu unamgusa mgongoni, anashtuka mno na kugeuka lakini hakuna anachokiona akawa anaoga kwa wasi wasi tele.baada ya kumaliza kuoga akachukua taulo na kuvaa, lakini ile taulo ilikuwa imelowa damu ila yeye hakuiona, akatoka na kuingia chumbani akasogea katika dressing table na kuanza kuupara, mara anaingia morey akiwa amevaa vizuri. Morey: vipi bado tu, mbona nguo yako imelowa damu? Nadya: damu ipo wapi? (huku akijitazama, morey anamuonesha katika ile taulo aliyoivaa, anaitoa na kuvaa khanga) Nadya: mbona mimi sijaumia hii damu imetoka wapi sasa? Morey: una uhakika na hilo lakini? (huku wakijaribu kuangalia angalia kama kuna jeraha sehemu yoyote lakini hawaoni kitu) Morey: mmh! Basi achana na hayo jiandae haraka twende. (nadya alianza kuwa na uwoga na hofu)
Scene 3 Wahusika: nadya na morey Mahali: ndani ya gari Muda: usiku Anaonekana akiwa mbali kimawazo nadya akiwa amegeukia nje akiwaza, morey hana habari anaendesha gari tu, nadya akatupa jicho katika kioo cha (middle mirror) kati ndani kuangalia nyuma akaona sura ya mtu nyuma akashituka na kupiga kelele ghafla, morey akapaki gari pembeni haraka sana. Morey: vipi kuna nini? Nadya: nimeona mtu kama, kama…….. Morey: kama nini, nadya una nini? (nadya anafungua mlango na kushuka huku akihema kwa wasi wasi na uwoga) Morey: tulia kwanza hayo ni mawazo tu, hebu twende kwanza kwa wazazi kisha tukirudi tutaongea vizuri. Nadya: hapana morey turudi nyumbani tu, kwani kuna jambo nataka nikwambie. (morey alimtazama nadya kwa makini kisha akashusha pumzi kali akamfungulia nadya mlango) Morey: ok, turudi nyumbani. (wanaingia kwenye gari na kugeuza kurudi nyumbani)
Scene 4 Mahali: nyumbani (sebuleni) Wahusika: nadya na morey Muda: usiku (anaonekana morey amesimama huku akiwaza jambo, nadya akiwa amekaa chini amejiinamia akiwaza wote wapo kimya hakuna anayeongea kitu) Morey: lakini ni jambo ambalo haliwezekani tumeshamzika mtu akifa amekufa. Nadya: kama huniamini sawa lakini imi nahisi na mambo yote hayo ninayokutana nayo ni yeye ndo anaye fanya miujiza hiyo. Morey: sikia nadya (huku anamsogelea na kumliwaza kwa maneno mbali mbali) Morey: hamna kitu kama hicho yeye ameshakufa na hawezi kurudi tena na zaidi hautakiwi kuamini juu ya mambo hayo…… Nadya: mi naogopa morey, natamani niende mbali Morey: hapana nadya, mapenzi yangu yote umeshayateka wewe nadya. Nadya: je watu wakijua itakuwaje? Morey: hamna atakaejua zaidi ya sisi watatu. Nadya: unamuamini kelvin? Morey: sio sana, lakini hamna atachojua juu yako kwani tumemzunguka labda umwambie wewe, mpenzi wake. (nadya akamtazama morey kwa hasira na majonzi kisha akainuka na kuondoka zake ndani, akamuacha morey pale sebuleni peke yake)
Scene 5 Wahusika: kelvin na mzimu wa shadya Mahali: nyumbani kwa kelvin Muda: usiku Akiwa amepumzika kwenye sofa hamna ajualo anatazama tv ghafla tv ikazimika, kila akijaribu kubonyeza hamna kitu akasogea karibu na tv kila akihangaika haiwaki, ghafla nyuma yake akahisi kama kuna mtu amepita alipogeuka hakumuona mtu alipata wasi wasi kidogo lakini alipuuza na kuendelea kukorokochoa hadi ikawaka akarudi kwenye sofa na kukaa, mara akaenda kwenye friji na kufungua akachukua kinywaji. Alipofunga ule mlango kuna kama mzimu alionekana kisha akapotea lakini kelvin hajui, akarudi katika sofa na kukaa akiendelea kutazama tv. Baada ya muda mfupi alikuwa ameshapitiwa na usingizi pale katika sofa akalala ndipo aliposikia sauti ya kicheko ambayo ilimshitua kelvin na kumpa hofu akainuka kwa woga akazima tv na kuingia chumbani huku akiogopa ogopa.
Scene 6 Mahali: ufukweni Wahusika: kelvin na wananchi Muda: asubuhi Wanaonekana wananchi wakiwa wanafanya mazoezi ya asubuhi kando na yanapopiga mawimbi kinaonekana kitanda kuna mtu kalala usingizi amejifunika habari hana . Baada ya kupigwa na mawimbi akaamka kwa kushtuka kumbe ni kelvin anashangaa kujikuta amelala ufukweni mwa bahari.watu wanaofanya mazoezi wanamshangaa Sound track kelvin: “nimefikaje hapa mimi si nililala nyumbani, hapa nimefikaje fikaje sasa …….!” Amebaki ameduwaa hajui lakufanya.
Scene 7 Wahusika: morey Mahali: juu ya ghorofa Muda: asubuhi (kukiwa kunapambazuka juu ya jengo moja refu (ghorofa) juu kabisa anaonekana morey akiwa amevaa nguo za kulalia, na amelala hana hata habari. Baada ya muda mfupi anaamka na kuanza kujishangaa kulala juu ya ghorofa, anakosa jibu anabaki anashangaa tu.
Scene 8 Wahusika: morey na nadya Mahali: sebuleni Muda: asubuhi Linaonekana gari ya kulipia (tax) imekuja na kusimama akashuka morey na kuingia ndani kisha akatoka na kumpa ela dereva , kisha yeye akarudi ndani na kukaa sebuleni akiwa anajiuliza maswali, mara anakuja nadya akashangaa. Nadya: morey ulikuwa wapi tangu usiku nakutafuta, umetoka hukuniambia kama unatoka , ulienda wapi, morey vipi? Morey: nimejikuta nimelala juu ya ghorofa Nadya: mbona sikuelewi? Morey alimtazama nadya usoni, na nadya akabaki anashangaa tu.
scene 9 Wahusika: morey, nadya na kelvin Mahali: sebuleni Muda: asubuhi Morey na nadya wanaonekana wakiwa kimya wamesimama kwa muda fulani mara kelvin anaingia wote wanamshangaa. Kelvin: habari zenu? Morey: safi, karibu. Kelvin: nina tatizo (anawatazama usoni nadya na morey) Morey na nadya wanatazamana pia. Nadya: tatizo gani? Kelvin: ananisumbua (wanatazamana tena usoni wote wakishanga, kelvin nae akawatazama kwa makini kina nadya.) Kelvin: shemeji shadya najua nimemkosea mdogo wako naomba uniombee kwa nadya anisamehe. (nadya akamtazama morey tena kwa mara nyingine, kisha morey akamtuliza kelvin) Morey: tulia kwanza tukae chini tuongee (wakakaa chini). Tatizo sio la peke yako. (kelvin akashangaa kidogo, akamtazama nadya ambae alikuwa amesimama) Nadya: lilianza kwangu (alizidi kushangaa na ukimya ukatanda)
Scene 10 Wahusika: morey na nadya Mahali: dukani Muda: mchana (wakiwa wanachagua nguo nadya alichukua nguo anazozitaka na kuweka kwenye mfuko, wakapanda gari na kurudi nyumbani)
Scene 11 Wahusika: morey na nadya Mahali: nyumbani Muda: mchana (wakiwa wamefika nyumbani, nadya akiwa na shauku ya kuona nguo alizokuja nazo akakaa chini na kufungua mfuko wake ili atoe zile nguo, lakini cha ajabu alitoa matambaa machafu ambayo yamechanika chanika! Alishangaa huku akitamani kucheka akiwa haelewi, morey akabaki ameduwaa hakuna aliyepata jibu.
Scene 12 Wahusika: morey na nadya Mahali: nyumbani Muda; mchana (wakiwa kimya kwa muda fulani) Morey: mimi nafikiri tunatakiwa kwenda kwa mtaalam ili haya mambo yaweze kutulia au unasemaje? (nadya hakujibu kitu alibaki kimya tu)
Scene 13 Wausika: morey, nadya na mtaalam Mahali: nyumbani Muda: jioni (wanashuka toka katika gari na kumkaribisha mtaalam ambae alibeba briefcase yake na usinga mkononi, amevaa suti nyeupe aliposhuka tu mtaalam mwili ukamsisimka, morey na nadya wote wakamtazama) Mtaalam: yupo humu humu ndani hayupo mbali. ( wakawa wanasogea mlangoni ghafla mlango ukafunguka wenyewe ndani wakatoka kuku na kukimbia, wakawa wanashangaa wakiwa wanasogelea mlango waingie ndani, mara mtaalam anaanguka na kufurukuta kama mtu mwenye kifafa, kisha akafa hapo hapo. Morey na nadya walizidi kupagawa hawakujua la kufanya.
Scene 14 Wahusika: morey na nadya Mahali: nyumbani (wanaonekana wakiingiza ile maiti chumbani, kisha wakarudi sebuleni wakiwa hawajui la kufanya) Nadya: sasa hii maiti tuipeleke wapi? Au tukaitupe? Na je polisi wakijua itakuwaje au tukaifukie? Morey: sasa mambo yote umemaliza mwenyewe, unaongea mwenyewe unajijibu mwenyewe hebu tulia kwanza. (ghafla wanasikia mlango wa chumba kimoja unafungwa kwa nguvu,wakashituka sana walielekea katika kile chumba na kufungua mlango kuangalia ndani hakuna kitu na ile maiti ilikuwa imepotea, wakabaki midomo wazi.
Scene 15 Wahusika: kelvin Mahali: nyumbani Muda: jioni (akiwa anasoma gazeti katika kuangalia habari za kwenye lile gazeti, aliiyona habari ya mtaalam wa mambo ya jadi akachukua namba za simu na kuanza kupiga, haikujulikana anaongea nae nini.
Scene 16 Wahusika: kelvin na morey Mahali: nyumbani Muda: usiku (wakiwa wapo katika mazungumzo yao) Kelvin: yeye ni mwanasaikolojia na ni profesa wa masuala ya kiasili amesomea katika chuo kikuu cha “scotland magistacy”.hivyo ni mtu mwenye uelewa mkubwa katika masuala ya viumbe visivyoonekana, nyota pamoja na kutatua matatizo hayo. Morey: unataka unambie ni mganga? Kelvin: ndiyo, ila sio wa matunguli na usinga kama wa hapa kwetu, yeye ni sawa na naturalist. Morey: mmh! Sawa tumtafute Kelvin: nimeshaongea nae inabidi tupange siku twende tukamuone tu. Morey: sawa, hamna tabu.
Scene 17 Wahusika: kelvin na watu kadhaa Mahali: bara barani Muda: usiku Tukio: ndoto (akiwa amevaa nguo za kulalia kelvin anaonekana kati kati ya bara bara akitembea peku peku huku mbele yake kuna watu wanne wamebeba sanduku la maiti huku wakiwa wamevaa nguo nyeusi tupu wengine wakisindikiza, walienda mbele kidogo kisha wakalishusha lile sanduku na kurudi kule walipotokea.walipishana na kelvin nae akawa anawashangaa wale watu kwanini wameshusha pale sanduku, hakuna aliyemuongelesha wala kumgusa walimpita.kelvin taratibu akasogea lilipo lile sanduku akiwa amejawa na hofu taratibu akaanza kulifungua, akakuta maiti iliyopo mle ina sura yake aliogopa na kupiga kelele.
Scene 18 Wahusika: kelvin Mahali:kitandani Muda: usiku (alishtuka kwa nguvu toka usingizini akiwa na mavazi yale ya kulalia akanza kuhema kwa hofu na uwoga)
Scene 19 Wahusika: morey, kelvin na profesa Mahali: ofisini Muda: asubuhi (wakiwa katika ofisi ya profesa huku wakimsikiliza kwa makini, profesa akiwa ameshika kipande cha kitambaa kina rangi tatu nyeupe,nyeusi na nyekundu akiwa anakichezesha chezesha) Profesa: kama mnajua bahati mbaya kwanini hamkutoa taarifa polisi? Morey: tulihofia kwani ni kesi kubwa sana ingetukabili Profesa: kwahiyo mmeogopa kesi mnakubali matatizo makubwa ok! Kama mlichagua hayo nyinyi wenyewe. Kelvin: hatuna maana hiyo, ndo maana tumekuja kwako utusaidie profesa. Profesa: mimi sina uwezo wa kuwasaidia mpaka upatikane ukweli Morey: ukweli upi huo tena zaidi ya huo?” (profesa aliwatazama kisha akainuka na kuwaambia wamfuate, ndipo wakatoka na kuingia kwenye chumba kimoja ambacho hakikuwa na kitu chochote zaidi ya kiti tu, ambacho kinaonekana cha muda mrefu na kipo kati kati ya chumba na pembeni kuna taa ya maajabu inayotumia mafuta.aliichukua ile taa na kuwapa kina kelvin pamoja na kibiriti.) Profesa:shikeni, tunataka kujua ukweli wa mambo, nitakaa kwenye kiti na kusafiri , nikishasafiri mimi atakuja mgeni, nitakapokuwa napishana nae taa itazimika na mwanaga utapotea, utahitajika mwanga wa asili ambao mtawasha hii taa, nimeeleweka vizuri. (kelvin na morey wakatazamana) Profesa akakaa kwenye kiti kisha wakamfunga mikanda, ndipo profesa akaanza kusoma kwa sauti ya chini baada ya muda mfupi akanza kubadilika, profesa alitumia nguvu nyingi na kutikisika kama anatetemeka , ghafla giza likaingia kuna sauti ya kukoroma ikawa inasikika. Kelvin: washa! Washa! (wakawasha taa na kumulika kwenye kiti ndipo walishangaa kuuona mzimu wa shadya umekaa pale ukikoroma, sauti nzito ya profesa) Mzimu: sitawasamehe hata kidogo lazima nitalipiza kisasi kwa kila mmoja wenu, hamkuona thamani ya uhai wangu, mkathamini yaliyo kwenye mioyo yenu………………………., lazima nilipe kisasi.
Kelvin: lakini ilkuwa bahati mbaya tu…. Mzimu: hakunaaaaa, tena wewe ndo msaliti mkubwa, unanisaliti kwenye kitanda changu…., sikusamehi, sikusamehiiiiiii. Hiiiiiiii, ghaaaaa, ngriiiiiiiiiii!!!!!!!!! (alianza kuunguruma kama simba ghafla taa ikazimika kukawa kama mwanzo, lakini cha ajabu profesa hakuwepo kwenye kile kiti, kilikuwa kitupu...
SIMULIZI MPYA YA “Kisasi Cha Usaliti” , SOMA HAPA UPATE RAHA.
4/
5
Oleh
Unknown
1 comments:
ITS good story are like it...........................................
Reply